COURSES OFFERED
St. Augustine Muheza Institute of Health and Allied Sciences
Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi ya Mtakatifu Augustino Muheza – Tanga (SAMIHAS) ambayo ina uzoefu wa kutoa elimu kwa wanataaluma wa afya kwa takribani miaka 80 sasa; inazo nafasi za mafunzo ya Stashahada ya Uuguzi na Ukunga (Diploma in Nursing and Midwifery) kwa mkupuo wa Machi 2020/2021. Aidha zipo nafasi za Stashahada ya Uuguzi na Ukunga; na Stashahada ya Afisa Tabibu (Clinical Officer) kwa mkupuo wa Septemba 2020/2021. Watakaokosa nafasi tunayo fursa ya kuwahamisha chuo cha Arcbishop John Ramadhani School of Nursing (AJRSN) kilichopo Korogwe. Wahi na fanya maombi sasa. Sifa za kujiunga ni kama ifuatavyo:-
Stashahada ya Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwifery)
Kozi za miaka (3) mitatu. Sifa kujiunga:- Ufaulu wa angalau "D" takika Fizikia, Kemia na Biolojia kwenye CSEE
Stashahada ya Utabibu (Clinical Officer)
Kozi za miaka (3) mitatu. Sifa kujiunga:- Ufaulu wa angalau "D" takika Fizikia, Kemia na Biolojia kwenye CSEE
Stashahada ya Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwifery) kwa Wanaojiendeleza
1. Kwa njia ya masafa(e-learning) kwa miaka miwili. 2. Kujiendeleza (In-service) kwa mwaka mmoja. Sifa za kujiunga:- Cheti cha Uuguzi na Ukunga (NTA L5) Ufaulu katika CSEE: 1.1. Ufaulu katika Fizikia, Kemia na Biolojia kwa wahitimu wa mmwaka 2010 hadi sasa. 1.2. Ufaulu wa somo moja la sanyansi kwa wahitimu wa kabla ya mwaka 2010.
Stashahada ya Utabibu (Clinical Officer) Kwa Wanaojiendeleza
Kozi za mwaka mmoja. Sifa za kujiunga:- Ufaulu wa angalau "D" katika Fizikia, Kemia na Biolojia kwenye CSEE. Cheti cha Utabibu cha NTA L5
Courses Offered
The programme enhances a wide range of study methods and approaches. They include lecture discussion, small group discussion, case studies, role plays, tutorials, assignments, practical training including demonstration, laboratory/ward attachment and study tours